• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KUTUNISHA MISULI: Muda wa usajili Mr Tanzania waongezwa

    (GMT+08:00) 2019-11-01 17:52:22
    Kamati ya shindano la Mr Tanzania, limesogeza mbele muda wa kuchukua fomu kwa ajili ya usajili baada ya mwitikio mkubwa wa vijana kutoka nje ya Jiji la Dar es Salaam wanaohitaji nafasi. Mkufunzi wa shindano hilo, Francis Mabugilo amesema, awali walipanga mwisho uwe Oktoba 30, lakini sasa mchakato wa kuchukua fomu utaendelea mpaka Novemba 26, siku ambayo usahili utafanyika na watakaoshinda wataingia kambini katika hoteli ya Serena. Amesema fainali za shindano hilo zitafanyika Novemba 29, mwaka huu Hyatt Regency.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako