• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaongeza ufanisi wa utawala kupitia ubora wa mfumo wa kisiasa

  (GMT+08:00) 2019-11-01 18:13:01

  Mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC umefungwa. Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika leo hapa Beijing, maofisa wandamizi wa serikali ya China wamesema, mkutano huo una maana kubwa, kwani umejibu swali muhimu kwamba, China inapaswa kushikilia, kuimarisha, kukamilisha na kuendeleza nini katika mfumo na utawala wa kitaifa.

  Mkutano huo wa siku nne ulimalizika jana mjini Beijing, baada ya kupitisha uamuzi kuhusu masuala kadhaa ya kushikilia na kukamilisha mfumo wa ujamaa wenye umaalumu wa China, na kuhimiza mambo ya kisasa katika mfumo na uwezo wa utawala. Rais Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa CPC alitoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo. Naibu mkuu wa idara ya uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa sera ya kamati hiyo Bw. Wang Xiaohui anasema,

  "Hii ni mara ya kwanza kwa Chama chetu kuitisha mkutano wa wajumbe wote ili kuchambua masuala ya mfumo na utawala wa kitaifa na kutoa uamuzi. Hivi sasa nchi yetu iko katika kipindi cha mseto cha malengo mawili ya miaka mia moja, huku tukikabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita duniani. Hivyo mkutano huo una maana maalum na ya kimkakati."

  Mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 18 ya CPC uliofanyikwa mwaka 2013 kwa mara ya kwanza ulitoa mada muhimu ya "kuhimiza mambo ya kisasa ya mfumo na uwezo wa utawala wa China". Baada ya juhudi za miaka zaidi ya mitano, ufanisi wa mageuzi katika nyanja muhimu umedhihirika. Kwenye mkutano uliofanyika jana, China imetoa lengo la jumla la kushikilia na kukamilisha mfumo wa ujamaa wenye umaalumu wa China, na kuhimiza mambo ya kisasa ya mfumo na uwezo wa utawala wa China, na pia imetoa mipango halisi ya kutimiza malengo hayo.

  Kuhakikisha mamlaka isitumiwe hovyo ni jambo muhimu kwa utawala wa taifa. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa sera ya Kamati Kuu ya CPC Bw. Jiang Jinquan amesema, mkutano huo umetoa maagizo matatu katika kushikilia, kuimarisha na kukamilisha mfumo wa uchunguzi wa kichama na kitaifa. Anasema,

  "Kupambana kithabiti na ufisadi kunatokana na dhamira ya CPC na mfumo wa ujamaa wa nchi yetu, na pia ni msimamo imara wa siku zote wa Chama chetu. Mkutano huo umezingatia kuimarisha na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya ufisadi, na kusisitiza kuondoa kabisa vitendo pamoja na mzizi wa ufisadi."

  Mkutano huo pia umetoa maamuzi kuhusu masuala mengine mbalimbali yakiwemo "nchi moja na mifumo miwili", na kufungua mlango zaidi katika mambo ya kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako