• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa Pareto watishia kuachana na kilimo cha zao hilo

    (GMT+08:00) 2019-11-01 18:13:15

    Baadhi ya wakulima wa pareto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya nchini Tanzania wametishia kuachana na zao hilo kwa madai kuwa halina faida kama ilivyo kwa mazao mengine ya biashara.

    Walidai kuwa wanatumia nguvu kubwa kuzalisha, lakini hakuna soko la uhakika kutokana na wanunuzi kuwa wachache ambao nao wanajipangia bei wanayoitaka isiyo na maslahi kwa wakulima.

    Baadhi ya wakulima hao walisema wana mpango wa kuanza kuyabadilisha mashamba wanayoyatumia kuzalisha zao hilo ili kupanda mazao mengine wakitaja miti.

    Kwa sasa wakulima wa zao hilo wana mnunuzi mmoja ambaye ni Pyrethrum Company of Tanzania (PCT) hali ambayo inafanya zao hilo kuuzwa bila ushindani na kufanya wakulima wasipate faida.

    Wameitaka serikali kuharakisha ujenzi wa kiwanda katika wilaya hiyo ili soko lipanuke kwa maelezo kuwa wanunuzi wa sasa wanapiga hesabu za usafirishaji kwenda Mafinga mkoani Iringa ambako ndiko kuna kiwanda.

    Alisema endapo kiwanda kitajengwa jirani na maeneo yao hata usafirishaji hautakuwa wa gharama kubwa na hivyo kuwafanya wauze kwa bei nzuri itakayotoa hamasa kwa wananchi kuendelea kulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako