• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni za China na Uingereza zasaini makubaliano ya awali kuongeza uwekezaji nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2019-11-01 20:17:58

  Kampuni za China nchini Kenya zimesaini makubaliano ya awali na Shirikisho la Wafanyabiashara la Uingereza tawi la Kenya (BCCK) kwa lengo la kuongeza uwekezaji katika sekta zinakazoboresha maisha ya jamii nchini humo.

  Hafla hiyo ilihudhuriwa na balozi wa China nchini Kenya Wu Peng, maofisa wa serikali ya Kenya pamoja na wafanyabiashara wakubwa, na ilirasimisha uratibu kati ya Jumuiya ya Uchumi na Biashara ya Kenya na China (KCETA), BCCK, na Muungano wa Sekta Binafsi nchini Kenya, (KEPSA).

  Makubaliano hayo ya pande tatu yatazingatia ushindani wa kampuni za China na Uingereza katika kuchochea uwekezaji kwenye sekta za kimkakati kama miundombinu, huduma za kifedha, uzalishaji na kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako