• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zambia yataka kupanua soko kwa kutumia fursa ya maonyesho ya CIIE

  (GMT+08:00) 2019-11-02 18:31:46

  Serikali ya Zambia imesema makampuni mengi ya nchi hiyo yanatarajia kupanua masoko kwa kutumia fursa ya Maonyesho ya pili ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa CIIE yatakayoanza Jumanne ijayo mjini Shanghai, China. Zambia ni nchi pekee mgeni wa heshima kutoka barani Afrika kwenye maonyesho hayo.

  Waziri wa biashara na viwanda wa Zmabia Bw. Christopher Yaluma akiwa ni kiongozi wa ujumbe wa makampuni ya Zambia kwenye maonyesho hayo, amesema maonyesho hayo yamevutia makampuni 40 ya Zambia´╝îikiwa ni pamoja na mashirika madogo na yenye ukubwa wa kati, na kuyapatia fursa ya kuingia kwenye soko la kimataifa.

  Bw. Yaluma ameisifu China kwa kuchukua hatua za kuzidi kufungua mlango wake, kitendo ambacho kitazipatia nchi nyingi fursa ya maendeleo, kuwapatia watu wengi zaidi nafasi za ajira, na kuboresha maisha ya watu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako