• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashirika ya wafanyabiashara ya China, Uingereza na Kenya yaimarisha ushirikiano nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2019-11-02 18:32:16

  Shirika la uchumi na biashara la China nchini Kenya, Shirika la biashara la Uingereza nchini Kenya na Muungano wa kampuni binafsi za Kenya, zilisaini kumbukumbu ya maelewano jana mjini Nairobi ili kukuza ushirikiano na kuhimiza uhusiano wa biashara wa kampuni za nchi hizo tatu.

  Kwenye hafla ya kusaini kumbukumbu hiyo, balozi wa China nchini Kenya Bw. Wu Peng alisema Kenya iko katika kipindi cha mwanzo cha kuendeleza viwanda vyake, ambapo kampuni za China zinaweza kuisaidia Kenya katika sekta za miundombinu na umeme. Balozi Wu alipongeza mashirika ya wafanyabiashara ya nchi tatu za China, Uingereza na Kenya kwa kuimarisha ushirikiano, kwani ushirikiano huo unalenga kuinufaisha Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako