Waziri wa viwanda na biashara wa Tanzania Bw. Innocent Bashungwa amesema Tanzania itatumia maonesho ya pili ya uagizaji wa bidhaa yatakayofanyika mjini Shanghai kutangaza bidhaa zake.
Bw. Bashungwa amesema Tanzania itaangalia ni nini inaweza kuuza kwa China na kwa nchi nyingine zitakazoshiriki kwenye maonesho hayo. Bw. Bashungwa ambaye ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye maonesho hayo amesema Tanzania itatangaza kuvutia uwekezaji kwenye sekta za kilimo, madini na uvuvi, na kuhimiza ushirikiano wa ubia kati ya wawekezaji wa China na Tanzania.
Amesema Tanzania ilinufaika na maonesho hayo ya mwaka jana kwa kupata ongezeko kubwa la watalii kutoka China, na takiwmu zinaonesha kuwa mwaka jana watalii elfu 30 wa China walitembelea Tanzania.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |