• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kuhimiza usawa wa kijinsia kwenye sekta ya nishati

  (GMT+08:00) 2019-11-02 18:33:33

  Kenya imezindua sera ya kuhimiza ushiriki wa wanawake na wasichana kwenye mnyororo wa thamani wa nishati wakati inafahamika kuwa umaskini, kutokuwa na ujuzi na imani za jadi zinawaweka wanawake nje ya sekta ya nishati.

  Katibu mkuu tawala wa wizara ya nishati ya Kenya Bw Simon Kachapin amesema Kenya ilikuwa ni nchi ya kwanza kuzindua sera inayozingatia jinsia kwenye sekta ya nishati. Amesema sera hiyo ina msingi wa kikatiba na ina lengo la kuhakikisha wanawake, wasichana, vijana na watu wanaoishi na ulemavu wanapata umeme sawa na watu wengine, na kusaidia kwenye mapambano dhidi ya umaskini na mabadiliko ya hali ya hewa.

  Katibu mkuu wa wizara ya nishati ya Kenya Bw Joseph Njoroge pia amesema Kenya itahimiza utekelezaji wa sera madhubuti zitakazohakikisha wanawake wanawakilishwa ipasavyo kwenye uongozi wa juu wa mashirika ya umeme.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako