• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Uingereza wathibitisha wahanga wote 39 waliokufa ndani ya lori ni raia wa Vietnam

  (GMT+08:00) 2019-11-02 18:48:14
  Polisi wa kaunti ya Essex ya Uingereza walitoa taarifa jana jioni kuwa wanaamini watu 39 waliofariki ndani ya lori mwezi uliopita nchini Uingereza wote walikuwa raia wa Vietnam.

  Kwa mujibu wa kamanda wa polisi anayeshughulikia kazi ya kuwatambua wahanga Bw. Tim Smith, alisema polisi wa Uingereza wanawasiliana na serikali ya Vietnam, na baadhi ya familia za wahanga zimethibitishwa. Wizara ya usalama ya Vietnam ilisema itapeleka tume ya kazi kwenda Uingereza ili kusaidia kutambua miili ya watu hao.

  Miili ya watu 39 iligunduliwa ndani ya konteina moja iliyochukuliwa na lori tarehe 23, Oktoba kwenye eneo la viwanda, kaunti ya Essex. Lori hilo lililoandikishwa nchini Bulgaria, liliinigia Uingereza kupitia bandari moja ya Welsh, na konteina ilitoka Ubelgiji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako