• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maoni: Kwenye ukweli uongo hujitenga

    (GMT+08:00) 2019-11-02 20:51:24

    Polisi wa kaunti ya Essex nchini Uingereza jana jioni walitoa taarifa kuwa wanaamini watu 39 waliofariki ndani ya lori mwezi uliopita nchini Uingereza wote walikuwa raia wa Vietnam. Ukweli huu unawahuzunisha watu, pia kofi la usoni kwa baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi, ikiwemo Shirika la CNN la Marekani.

    Wakati uraia wa wahanga hao haujathibitishwa wala hali halisi ya tukio hilo haijafahamika, Shirika la CNN lilipata majibu linayoyataka, likiiuliza wizara ya mambo ya nje ya China, "je, kwa nini hao raia wa China walikimbia China kwa kutumia njia hiyo ya ajabu kabla ya maadhimisho ya miaka 70 ya kuzaliwa kwa Jamhuri ya watu wa China?" Swali hilo si kama tu halina msingi wowote, bali pia linakosa huruma wa kimsingi kwa ubinadamu. Na kabla ya hapo, CNN inayojitangaza kutoa habari kwa uhuru, ililazimika kuomba radhi kutokana na kutoa habari feki kuhusu polisi wa Hong Kong kutumia mabomu ya machozi.

    Ukweli uliobainika wa tukio hilo la Essex umeifanya CNN ijidhihaki. Shirika hilo linalojitangazia kutoa habari kwa uwiano, kumbe linavaa miwani ya rangi huku likiwa bado linashikilia mawazo ya vita baridi. Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi, kama CNN, vinaamua kufumbia macho matatizo ya nchi zao zenyewe, na kukaa kimya kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika nchi zinazoendela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako