• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China ahudhuria mkutano wa 18 wa Baraza la viongozi wa serikali za nchi wanachama wa SCO

  (GMT+08:00) 2019-11-03 18:03:35

  Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang jana alihudhuria mkutano wa 18 wa Baraza la viongozi wa serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO mjini Toshkent nchini Uzbekistan.

  Akitoa hotuba kwenye mkutano huo Bw. Li amesema mafanikio mengi ya ushirikiano yamepatikana katika miaka 18 tangu shirika la SCO lianzishwe. Kwa sasa mabadiliko yenye utatanishi yametokea duniani na kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia imepungua. Nchi wanachama wa shirika hilo zinapaswa kuhimiza mshikamano na uaminifu, na kukabiliana na chamgamoto kwa pamoja. Ametoa mapendekezo kwamba nchi wanachama wa shirika hilo zinatakiwa kuimarisha uwezo wa kujilinda kiusalama, kupanua nafasi za maendeleo, kuzidisha mawasiliano, kuongeza nguvu mpya ya maendeleo yenye uvumbuzi, na kunufaika pamoja na mafanikio.

  Wakati huohuo, Bw Li Keqiang amekutana na mwenzake wa Kazakhstan Bw. Askar Uzakbaiuly Mamin mjini Toshkent.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako