• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Askari wa Somalia na AU kuboresha shughuli zinazohusisha jeshi na umma

  (GMT+08:00) 2019-11-03 18:04:56

  Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM na Jeshi la Taifa la Somalia SNA wamekamilisha mafunzo ya pamoja juu ya kuboresha shughuli zinazohusisha jeshi na umma ili kusaidia kuimarisha uhusiano na jamii mbalimbali za maeneo yaliyokombolewa.

  Ikitoa taarifa jana AMISOM imesema mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika Jowhar yamelenga kutoa taratibu zinazoongoza uhusiano kati ya watu wa misaada ya kibinadamu, raia, na vikosi vya usalama. Taratibu hizo zinabainisha jinsi jeshi na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanavyotakiwa kujihusisha katika maeneo ya migogoro ili kuweza kufikisha misaada ya kibinadamu kwenye jamii zenye mahitaji.

  Mafunzo hayo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yalihudhuriwa na maofisa wa ushirikiano wa kijeshi waliopelekwa kutoka kikosi cha AMISOM cha Burundi na askari wa SNA ambao wapo kwenye opresheni ya pamoja na AMISOM.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako