• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika Kusini yaahidi kufanya mageuzi haraka ya kiuchumi

  (GMT+08:00) 2019-11-03 18:05:18

  Serikali ya Afrika Kusini jana iliahidi kuendeleza mageuzi muhimu ili kuboresha utendaji wa kiuchumi kufuatia nchi hiyo kushushwa hadhi yake ya kukopa kutoka hali ya kawaida hadi hasi.

  Kwenye taarifa iliyotolewa na Hazina ya taifa baada ya shirika la kimataifa Moodys la kuweka viwango kushusha kiwango cha kukopa cha Afrika Kusini kutoka cha kawaida hadi hasi, imesisitiza kuwa mageuzi ya kiuchumi ni lazima yatekelezwe bila kuchelewa, kwani serikali inafahamu kwamba mageuzi ya muda mrefu na muda mfupi yanahitajika haraka ili kuboresha utendaji wa kiuchumi katika miaka kadhaa ijayo.

  Mashirika mengine mawili ya kuweka viwango S&P Global Rating na Fitch yameweka uaminifu wa kukopa wa Afrika kusini kwenye kiwango cha chini cha uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako