• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jumba la Afrika Kusini kwenye maonesho ya CIIE lafunguliwa Shanghai

  (GMT+08:00) 2019-11-04 08:22:57

  Jumba la Afrika Kusini kwenye Maonesho ya pili ya Uagizaji Bidhaa ya Kimataifa ya China CIIE limefunguliwa mjini Shanghai, na mhazini mkuu wa chama cha ANC Bw. Paul Mashatile alikata utepe wa uzinduzi wa jumba hilo.

  Bw. Mashatile amesema kupitia majukwaa muhimu ikiwemo "Ukanda mmoja, Njia moja", Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na maonesho haya ya CIIE, China imetoa uzoefu wa fursa za maendeleo kwa Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika, na kuisaidia nchi hiyo kuingia kwenye njia ya maendeleo ya kasi. Amesema, Afrika kusini na China kwa sasa ziko kwenye kipindi kizuri cha maendeleo ya uhusiano kati yao, na Afrika kusini inapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano na China kwenye nyanja mbalimbali, hususan katika sekta ya uchumi na biashara.

  Ofisa huyo amesema kuanzishwa kwa jumba hilo kunalenga kuweka mnara mpya wa ushirikiano wa kunufaishana kati ya Afrika Kusini na China, na kuhimiza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako