• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yateua majaji 12 ili kuboresha uendeshaji wa kesi

  (GMT+08:00) 2019-11-04 08:41:33

  Rais John Magufuli wa Tanzania ameteua majaji 12 wa mahakama kuu ili kuboresha uendeshaji wa kesi. Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu imesema majaji hao wanaapishwa leo.

  Mwezi Februari mwaka jana, Rais Magufuli alitaja baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanyika ili kuboresha utendaji wa mahakama, na kumtaka jaji Mkuu Ibrahim Juma kuwachunguza mahakimu wanaofanya ziara za mara kwa mara kwa mapumziko barani Ulaya, na kutaka kujua wanapata wapi pesa kwa ajili ya safari hizo.

  Pia alisema hatua stahiki zinatakiwa kuchukuliwa dhidi ya wafanyakazi mafisadi wa mahakama, ili kuboresha sura ya mahakama za Tanzania na kuwa watu kama hao hawana nafasi kwenye serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako