• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la Syria lajiimarisha kaskazini mwa Syria

  (GMT+08:00) 2019-11-04 08:41:59

  Jeshi la Syria limeimarisha nafasi yake kwenye maeneo ya jimbo la Hasakah kaskazini mwa Syria na kukutana na vikosi vyake vinavyosonga mbele kutokea jimbo la Raqqa.

  Taarifa iliyotolewa inasema hatua hiyo ya jeshi la Syria inatokana na majukumu ya kukabiliana na uvamizi wa Uturuki. Kupangwa huko kwa vikosi kwenye maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wa kikurd, kunatokana na makubaliano yaliyofanikishwa na Russia mwezi uliopita.

  Kuwekwa kwa vikosi hivyo kwenye jimbo la Hasakah na kuvifikia vikosi vyake vya Raqqa, kunachukuliwa kama ni njia ya kufungua njia za ugavi za ardhini tangu mwaka 2012, kabla ya hapo shughuli za ugavi zilifanyika kwa njia ya ndege.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako