• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Lewis Hamilton atia kibindoni taji lake la sita duniani la udereva kwenye mbio za US Grand Prix

  (GMT+08:00) 2019-11-04 08:45:35

  Lewis Hamilton ametia kibindoni taji lake la sita la udereva duniani akimaliza nafasi ya pili kwenye mbio za United States Grand Prix. Matokeo hayo yanamaanisha Hamilton anakuwa dereva wa pili wa Formula 1 mwenye mafanikio zaidi katika muda wote akimsogelea kwa karibu mno bingwa wa muda wote anayeshika rikodi Michael Schumacher, ambaye amekwaa mataji saba. Hamilton ameshindwa baada ya kupambana kishujaa na kutaka kunyakua ushindi kwa kujaribu mbinu tofauti dhidi ya dereva mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas lakini hilo halikuwa tatizo hata kidogo kwani alikuwa na faida ya pointi. Hamilton alimzuia Max Verstappen na kuwa wa pili huku Bottas akiondoka na ushindi. Taji la sita la Hamilton pia limempaisha na kumpita legendary Argentine Juan Manuel Fangio. Hamilton amepata ubingwa baada ya kushinda mbio 10 kati ya 19 za msimu huu, akiwa amebakisha mbili za Brazil na Abu Dhabi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako