• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bayern Munich yapeana mkono wa kwaheri na kocha wao Niko Kovac kufuatia kushindwa 5-1 Eintracht Frankfurt

  (GMT+08:00) 2019-11-04 08:45:59

  Klabu ya FC Bayern Munich imetangaza rasmi kumtimua kazini aliyekuwa kocha wao Niko Kovac mwenye umri wa miaka 48, siku moja tu baada ya kufungwa magoli 5-1 dhidi ya Frankfurt. Kovac raia wa Croatia anaondoka akiwa kashindwa kufikia malengo ya klabu hiyo na sasa anaondoka Bayern ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo kwa kuwa na point 18, hizo zikiwa ni alama nne nyuma ya vinara Borussia Monchengladbach. Bayern Munich ikiwa chini ya Kovac ndani ya Bundesliga msimu wa 2019/20, imecheza jumla ya mechi 10, imeshinda mechi 5, sare 3 na wamepoteza mechi 2 na kama wangeshinda dhidi ya Frankfurt wagekuwa nafasi ya pili. Kwenye taarifa yake Bayern imesema uamuzi huo umekuja baada ya makubaliano ya pande mbili na Niko Kovac jana Jumapili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako