Klabu ya Yanga SC ya Tanzania imemaliza safari yake ya michuano ya kimataifa usiku wa Novemba 3 2019 nchini Misri baada ya kucheza mchezo wake wa marudiano wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga SC waliingia katika uwanja wa June 30 kurudiana na Pyramids wakiwa nyuma kwa magoli 2-1, magoli ambayo yalifungwa katika mchezo wa kwanza uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kwa kipigo hicho cha 3-0 Yanga sasa wanaondoka rasmi katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 5-1 na kuungana na Simba, KMC na Azam Fc zilizotolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho. Kufunga magoli mawili bila kuruhusu kufungwa goli ilikuwa ngumu zaidi na kujikuta wakimaliza mchezo huo kwa kufungwa kwa magoli 3-0, magoli ya Pyramids FC yakifungwa na Traory dakika ya 27, Farouk 79 na El Said dakika za nyongeza, kwa maana hiyo Tanzania sasa msimu wa 2019/20 haina muwakilishi yoyote wa kimataifa katika michuano hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |