• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Li Keqiang ahudhuria mkutano wa 22 wa wakuu wa China na Jumuiya ya nchi za Asia Kusini Mashariki

    (GMT+08:00) 2019-11-04 09:00:22

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana asubuhi alihudhuria mkutano wa 22 wa wakuu wa China na Jumuiya ya nchi za Asia Kusini Mashariki ASEAN uliofanyika huko Bangkok nchini Thailand.

    Kwenye mkutano huo Bw. Li Keqiang amesema, siku zote China inaunga mkono hadhi kuu ya ASEAN kwenye ushirikiano wa Asia Mashariki. China na ASEAN zinaheshimiana, kutendeana kwa usawa, kutatua migongano kwa njia ya mazungumzo, na kulinda amani na utulivu wa kikanda kwa pamoja. Bw. Li amezitaka pande hizo mbili zishikilie njia ya kupata maendeleo ya pamoja, na kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yao.

    Wakuu wa nchi za jumuiya hiyo wamesifu maendeleo ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika mwaka uliopita, na wamesema nchi za Asia Kusini Mashariki zinapenda kushiriki kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kulinda pamoja siasa yenye pande nyingi na biashara huria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako