• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa shirika la UM waanza UAE kukuza maendeleo ya kiviwanda

    (GMT+08:00) 2019-11-04 09:15:50

    Kikao cha 18 cha Mkutano Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO kimeanza mjini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu UAE. Kikao hicho kitaangalia nafasi muhimu ya maendeleo shirikishi na endelevu ya viwanda katika kutimiza Ajenda ya 2030, haswa chini ya mazingira ya Mapinduzi ya Nne ya Kiviwanda. Mkurugenzi mkuu wa UNIDO Li Uong amesema kwenye hotuba yake ya ufunguzi kwamba inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2030, viwanda vitakuwa shirikishi na endelevu, na vitakuza uchumi usiochafua mazingira na unaoendana na tabianchi, ambao utatoa nafasi bora za ajira, ukuaji shirikishi, ustawi wa pamoja na kuwawezesha watu wote katika nchi zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako