• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la anga la Nigeria lashambulia maficho ya kundi la Boko Haram

  (GMT+08:00) 2019-11-04 17:33:06

  Jeshi la anga la Nigeria limeshambulia na kuharibu moja ya maficho ya kundi la kigaidi la Boko Haram katika mkoa wa Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

  Msemaji wa jeshi hilo Ibikunle Daramola aliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, maficho hayo yaliyoshambuliwa yako kando ya Mto Chad katika mkoa huo, na kuongeza kuwa, operesheni hiyo pia ilisababisha vifo vya wapiganaji kadhaa wa kundi hilo.

  Amesema taarifa za kiintelijensia zimesema, kundi hilo lilitumia sehemu hiyo kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama. Pia amesema, jeshi hilo kwa kushirikiana na majeshi ya ardhini, litaendelea kushambulia maeneo yaliyobaki ya wapiganaji wa Boko Haram.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako