• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonyesho ya CIIE yafungua mlango kwa zao la parachichi kutoka Kenya

  (GMT+08:00) 2019-11-04 19:06:37

  Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Uingizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE) yatafunguliwa kesho mjini Shanghai, na yatafungua mlango kwa zao la parachichi kutoka Kenya, ambayo ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa parachichi barani Afrika.

  Kwenye mkutano wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika mwezi Aprili mwaka huu, China na Kenya zilisaini makubaliano kuhusu vigezo vya ukaguzi na upimaji wa parachichi za Kenya zitakazouzwa nchini China, hivyo kuifanya Kenya iwe nchi ya tano duniani na nchi ya kwanza barani Afrika kuruhusiwa kuuza parachichi nchini China.

  Kansela wa biashara kutoka ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Guo Ce amesema, ndani ya mwaka mmoja, China na Kenya zimesaini makubaliano ya uagizaji wa aina tatu za mazao ya kilimo ya Kenya, na makampuni 15 ya Kenya kutoka sekta za utalii na vyakula yatashiriki kwenye maonyesho ya mwaka huu, jambo lenye maana kubwa kwa Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako