• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa majaji

  (GMT+08:00) 2019-11-05 08:44:13

  Jaji mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma amesema Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa majaji, na kuathiri utekelezaji wa sheria nchini humo.

  Akiongea Ikulu nchini Tanzania muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kuwaapisha majaji 12 aliowateua jumapili, Jaji Ibrahim Juma amesema kwa sasa majaji wachache wanashughulikia kesi 518 kwa mwaka, wakati kiwango cha kawaida kinatakiwa kuwa kesi 220 kwa mwaka.

  Kuapishwa kwa majaji hayo kumefanya idadi ya majaji nchini Tanzania kufikia 78. Hata hivyo Jaji Ibrahim Juma amesema kati ya majaji hao 78 wawili wamepewa kazi maalum, na wengine wawili watastaafu mwaka huu, na kufanya idadi ya majaji kuwa 74. Kwa hiyo amemuomba Rais Magufuli ateue majaji zaidi ili kuziba nafasi hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako