• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viongozi wa biashara wa Kenya wana matumaini na maonesho ya pili ya CIIE ya China katika kuhimiza biashara

  (GMT+08:00) 2019-11-05 08:44:49

  Viongozi wa biashara wa Kenya wana matumaini kuwa maonesho ya pili ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China CIIE yatasaidia kutangaza zaidi bidhaa za Kenya kwenye soko la China, ikiwa ni pamoja na chai, kahawa, maua, viungo na maparachichi, bidhaa ambazo zinaongoza katika kuiletea Kenya mapato ya fedha za kigeni.

  Makampuni kadhaa ya Kenya yanapanga kushiriki kwenye maonesho hayo yanayofanyika mjini Shanghai. Kaimu mtendaji mkuu wa Chama cha wafanyabiashara na wanaviwanda wa Kenya Bw. George Kiondo, amesema maonesho hayo yanafanyika wakati China na Kenya zinafanya juhudi ya kuimarisha mahusiano kati ya pande mbili na mahusiano ya biashara.

  Pia amesema kupitia maonesho hayo, Kenya itajifunza mambo ya uzalishaji viwandani hasa kwenye upande wa ongezeko la thamani, na kujenga uwezo ili waweze kuzalisha bidhaa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako