• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka jumuiya ya kimataifa izisaidie nchi za pembe ya Afrika kutimiza amani na maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-11-05 09:03:11

    Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Wu Haitao jana kwenye mkutano wa Baraza la usalama alitoa hotuba kuhusu masuala ya wanawake, amani na usalama katika pembe ya Afrika, akiitaka jumuiya ya kimataifa izisaidie nchi za pembe kuleta amani na maendeleo, na kulinda haki na maslahi ya wanawake.

    Balozi Wu amesema China na Afrika siku zote ni jumuiya yenye hatma ya pamoja. China inaunga mkono juhudi za nchi za Afrika za kulinda amani na utulivu wa kikanda, na inapenda kushirikiana na nchi za Afrika na jumuiya ya kimataifa kuhimiza maendeleo ya kazi za Umoja wa Mataifa kwenye sekta za wanawake, amani na usalama, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya amani na maendeleo ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako