• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati kuimarisha ushirikiano ili kuhakikisha usalama wa mipaka

  (GMT+08:00) 2019-11-05 09:03:37

  Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati jana zimefikia makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya kijeshi, na kuhakikisha usalama wa mipaka kwa njia ya kuweka jeshi la pamoja.

  Mwenyekiti wa baraza la utawala nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan, jana huko Khartoum alifanya mazungumzo na waziri wa ulinzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Bw. Marie Nolle Koyara ambaye yuko ziarani nchini Sudan. Kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao, waziri wa ulinzi wa Sudan Bw. Gamal al-Din Omer, amesema Sudan na Jamhuri ya Afrika zitaweka jeshi la pamoja kwenye eneo la mpaka kati ya Sudan, Chad na Jamhuri ya Afrika ili kuhakikisha usalama wa kanda hiyo.

  Bw. Omer pia amesema nchi hizo mbili pia zimekubaliana kutumia raslimali kadiri iwezekanavyo ili kutatua changamoto za kiuchumi zinazolikabili eneo hilo, na kuwanufaisha wananchi wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako