• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Cardiff City kukabiliwa na marufuku katika madirisha matatu ya uhamisho kama watashindwa kuilipa Nantes

  (GMT+08:00) 2019-11-05 09:30:59

  Cardiff City watakabiliwa na marufuku katika madirisha matatu ya uhamisho kama watashindwa kuilipa Nantes awamu ya kwanza ya ada ya uhamisho wa mshambuliaji marehemu Emiliano Sala kiasi cha £15m. Sala, aliyekuwa na miaka 28, amefariki kwenye ajli ya ndege Januari wakati akisafiri kutoka Ufaransa kwenda kujiunga na klabu yake mpya. Fifa imetoa sababu kamili ilipoiamuru Cardiff kulipa awamu ya kwanza 6m euros (£5.3m) mwezi Septemba. Cardiff itawasilisha rufaa yake dhidi ya uamuzi huo katika wiki mbili zijazo kwenye mahakama ya Usuluhishi wa Michezo. Klabu hiyo bingwa inasema kwamba haiwajibiki na ada yoyote kwasababu Muargentina huyo hakuwa mchezaji wao rasmi wakati anafariki. Lakini kamati ya hadhi ya wachezaji ya FIFA PSC imeilazimisha Cardiff kulipa pesa za awamu ya kwanza walizokubaliana kwenye uhamisho na kuikatalia klabu hiyo kutolipa kwa sababu mbalimbali. PSC pia imetupilia mbali madai ya Cardiff kwamba mkataba wa Sala na Nantes ulikuwa bado haujavunjwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako