• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwanariadha wa Uholanzi Madiea Ghafoor ahukumiwa kwenda jela kwa kujihusisha na magendo ya dawa za kulevya

  (GMT+08:00) 2019-11-05 09:18:14

  Mwanariadha kutoka Uholanzi Madiea Ghafoor amehukumiwa kifungo cha miaka minane na nusu baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha na kufanya magendo ya dawa za kulevya. Ghafoor mwenye miaka 27 ambaye alishiriki Olimpiki ya Rio mwaka 2016 katika mbio za kupokezana vijiti 4x400m, alibambwa akiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya £2m kwenye buti lake la gari wakati aliposimamishwa mpakani karibu na Elten nchini Ujerumani kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida mwezi Juni. Alikuwa na kg 50 za vidonge vya ecstasy, kg 2 za crystal meth na pesa taslim euro 11,950. Hata hivyo mwanariadha huyo jana akiwa kwenye mahakama ya wilaya ya Kleve, aliashiria kuwa huenda akakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, huku akikana kuwa hana hatia. Mahakamani alisema alifikiri amebeba dawa za kusisimua misuli na hakujua kuwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya ecstasy na crystal meth. Pia alikataa kumtaja aliyempa dawa hizo na kusema anaihofia familia na rafiki zake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako