• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nadal arejea kuwa namba moja duniani licha ya Djokovic kushinda Paris

    (GMT+08:00) 2019-11-05 09:18:36

    ATP jana ilitaja viwango vipya kwa wachezaji wa tenisi na kumtaja Rafael Nadal kuwa tena namba moja duniani kwa mara ya nane katika kibarua chake cha mchezo wa tenisi. Mhispania huyo amemchupa Novak Djokovic ingawa amepata taji lake la tano katika Paris Masters siku ya Jumapili kwa ushindi wa 6-3, 6-4 dhidi ya Mcanada Denis Shapovalov. Nadal, ambaye aliitema nafasi hiyo ya namba moja Novemba 4, 2018, alijitoa kwenye nusu fainali dhidi ya Shapovalov huko Paris kutokana na kukazwa na misuli ya tumbo. Naye Djokovic ameporomoka kwenye viwango kwasababu amepoteza pointi alizoshinda mwaka mmoja uliopita huko London wakati Nadal hayupo. Mpambano wa mwaka 2019 kati ya Nadal, mshindi wa michuano ya wazi ya Ufaransa na Marekani na Djokovic aliyebeba ushindi Australia na Wimbledon, ulikuwa mkali na kuibua kitendawili kwamba nani atamaliza mwaka akiwa namba moja. Nadal alichukua nafasi ya namba moja kwa mara ya kwanza August 18, 2008 wakati ana miaka 22 tu. Alidumu kwenye nafasi hiyo kwa wiki 197, na kuwa namba sita kushikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu katika historia ya ATP akiwa nyuma ya Roger Federer (310), Pete Sampras (286), Djokovic (275), Ivan Lendl (270) na Jimmy Connors (268).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako