• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mario Balotelli akasirishwa na ubaguzi aliofanyiwa na mashabiki wa Verona

  (GMT+08:00) 2019-11-05 09:19:18

  Mshambuliaji nguli wa Brescia, Mario Balotelli ameonja shubiri baada ya mashabiki wa klabu ya Verona kumdhihaki kwa kumuita nyani uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu Italia ambao Verona ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Brescia. Akionyesha kukasirishwa na kitendo hicho Balotelli alipiga mpira kwenda kwa mashabiki jukwaani, kabla ya kuchukua uamuzi wa kutoka uwanjani. Kocha wa Verona, Ivan Juric alidai Balotelli hakufanyiwa vitendo hivyo licha ya picha za televisheni kumuonyesha akitoka nje kwa hasira dakika ya 54 baada ya kupiga mpira kwa mashabiki. Baadhi ya wachezaji wa Verona na Brescia walimsihi asitoke uwanjani. Kwenye Instagram yake Balotelli aliposti ujumbe akimjibu mkuu wa Verona Luca Castellini, aliyesema kuwa Balotelli ni Muitaliana kwasababu ana uraia wa Italia, lakini hawezi kuwa Muitaliana halisi, kwamba wanajiingiza kwenye hali ya kijamii na kihistoria ambayo hata hawaielewi, na kuwaita watu wenye mtazamo finyu. Hata hivyo Castellini amesema hivi karibuni walimsaini mchezaji mweusi na Verona nzima ilimpongeza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako