• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bandari ya Lamu iliyojengwa na kampuni ya China kupokea meli ya kwanza Disemba

  (GMT+08:00) 2019-11-05 09:42:20

  Bandari iliyojengwa na kampuni ya China katika kisiwa cha Lamu nchini Kenya inatarajiwa kuzinduliwa mwezi Disemba mwaka huu.

  Meneja mkuu wa Mamlaka ya Bandari ya Kenya KPA Bw. Daniel Manduku, amesema bandari hiyo iliyojengwa na Kampuni ya China CCCC itapokea meli ya kwanza kutoka Maersk mwezi ujao, na itakuwa kitovu cha usafirishaji wa mizigo baharini kwa sehemu kama vile Dar es Salaam, Zanzibar na Maputo. Ameongeza kuwa bandari ya Lamu itakamilisha uwezo wa bandari iliyopo ya Mombasa, kurahisisha usafirishaji wa mizigo inayoingia na kutoka Kenya na nchi jirani, na kuimarisha hadhi ya Kenya kuwa kitovu cha kikanda cha usafirishaji baharini.

  Aidha, Bw. Manduku amesema Kenya itashirikiana na China katika shughuli za bandari ili kuhimiza biashara ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako