Maonesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa China yamefunguliwa leo mjini Shanghai, China. Rais Xi Jinping wa China amehutubia ufunguzi huo.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya "zama mpya, kunufaika kwa pamoja na mustakabali wa pamoja" yameshirikisha zaidi ya makampuni 3,000 kutoka nchi na sehemu 150 za mabara matano duniani.
Viongozi wa nchi kadhaa akiwemo rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Bw. Roberto Azevedo wamehudhuria ufunguzi huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |