• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jepkosgei atamani kuvunja rekodi ya mbio za marathon

    (GMT+08:00) 2019-11-05 18:30:14

    Mwanariadha Joyciline Jepkosgei amefichua azma ya kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za kilomita 42 baada ya kuibuka mshindi wa New York Marathon, Amerika mnamo Jumapili. Rekodi ya dunia katika mbio za marathon kwa wanawake kwa sasa inashikiliwa na Mkenya Brigid Kosgei ambaye amepania kubadilisha uraia na kuanza kupeperusha bendera ya Amerika baada ya Michezo ya Olimpiki itakayoandaliwa jijini Tokyo, Japan mwaka ujao. Jepkosgei ambaye kwa sasa ni mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za kilomita 21, alikuwa akishiriki mbio za marathon kwa mara ya kwanza. Alikamilisha mbio za wikendi iliyopita kwa muda wa saa 2:22:38. Kwa upande wa wanaume, Mkenya Geoffrey Kamworor aliibuka mshindi wa marathon kwa mara ya pili chini ya kipindi cha miaka mitatu, akikamilisha mbio za Jumapili uwanjani Central Park kwa muda wa saa 2:08:13 na kukumbatiwa na bingwa wa Olimpiki na Dunia Eliud Kipchoge, ambaye amekuwa akifanya naye mazoezi ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako