• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bonanza la siku ya Takwimu Afrika lashika kasi

  (GMT+08:00) 2019-11-05 18:30:34
  Bonanza la michezo kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika limeendelea tena kwa kupigwa michezo mitatu tofauti katika uwanja wa Mao Zedong. Kwa upande wa mpira wa miguu, kulikuwa na mechi mbili kati ya timu ya Mamlaka ya Manunuzi dhidi ya Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wanawake na Watoto. Katika mchezo huo timu ya Mamlaka ya Manunuzi ilifanikiwa kuibuka na ushindi kwa kuifunga Wizara ya Wanawake mabao 6-1. Pambano jingine liliwakutanisha Mthibiti wa Hesabu za Serikali dhidi ya Wizara ya Biashara, ambapo timu ya Mthibiti iliibuka na ushindi mabao 5-0. Mbali na michezo hiyo pia kulifanyika mchezo wa kuvuta kamba kwa kuwakutanisha Mamlaka ya Manunuzi dhidi ya Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wananwake na Watoto, ambapo Mamlaka ya Manunuzi ilifanikiwa kushinda kwa kuwavuta Wizara ya Kazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako