Kocha wa Mwadui FC Khalid Adam amesema timu yake ityafanya juu chini kupata ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kesho kwenye Uwanja mpya wa Gairo mkoani Morogoro. Amesema kila mechi kwake ni sawa na fainali, na amewaandaa vema wachezaji wake kupambana na kuhakikisha wanafanya vema katika mchezo huo na kusahau matokeo ya nyuma. Tayari timu hiyo imeshafika Morogoro kwa ajili ya mchezo huo.