• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawimbi ya runinga kutumika kupeleka huduma ya intaneti vijijini

    (GMT+08:00) 2019-11-05 20:26:28
    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Mhandisi Isack Kamwelwe, ameelekeza mawimbi ya runinga yatumike kupeleka huduma ya intaneti vijijini ili jamii iweze kutumia mawimbi hayo kupata huduma ya mawasiliano ya intaneti.

    Kamwelwe aliyasema hayo wakati akikagua mnara wa mawasiliano, Kondoa Mjini ambao umefungwa vifaa maalum kwa ajili ya kubeba mawimbi ya runinga na kupeleka kwenye kifaa kingine ambapo mawimbi hayo yanabadilishwa na kuweza kutumika kutoa huduma ya intaneti kwenye jamii ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kondoa, Shule ya Sekondari ya Ura na Chuo cha Ualimu cha Bustani zilizopo wilayani Kondoa, Dodoma.

    Kongamano hilo lililofanyika kwa muda wa siku 6 kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa ambalo lilianza Oktoba 28, 2019 na kumalizika Novemba 2, 2019.

    Wakati Kamwelwe akikagua mnara huo, Mkufunzi Msaidizi wa UDOM, Jabhera Matogoro, alimweleza kuwa mawimbi kwa ajili ya runinga yanasafiri umbali wa kipenyo kizichozidi kilomita 20 ambapo baadhi ya maeneo hayafikiwi na mawimbi hayo ambapo kiasi kikubwa cha mawimbi yanabaki bila kutumika ipasavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako