• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar yatafuta ushirikiano zaidi na Korea Kusini

  (GMT+08:00) 2019-11-05 20:26:45
  Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ameipongeza Korea Kusini kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kusisitiza haja ya kuwapo ushirikiano katika sekta ya utalii baina ya pande mbili hizo.

  Dk. Shein aliyasema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Cho Taeick.

  Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimweleza Balozi huyo kuwa Zanzibar imeweza kuimarika katika sekta ya utalii kutokana na vivutio kadhaa vilivyopo sambamba na mikakati madhubuti iliyowekwa.

  Aliongeza kuwa katika kuhakikisha uhusiano na ushirkiano unaimarika zaidi kati ya pande mbili hizo hasa katika sekta ya utalii, iko haja ya kuwapo ushirikiano kati ya Zanzibar na kisiwa cha Cheju nchini Korea ambacho ni maarufu duniani kwa utalii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako