• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda na Volkswagen zafanyia majaribio gari linanotumia umeme

    (GMT+08:00) 2019-11-05 20:27:06
    Rwanda inashirikiana na kampuni ya kutengeneza magari Volkswagen kutoka ujerumani kufanyia majaribio gari aina ya Golf linanotumia umeme.

    Ushirikiano huo unalenga kupunguza utoaji wa gesi chafu na pia unaendana na mapango wa kampuni ya Volkwagen wa kuacha kutengeneza magarai ya mafuta mwaka 2030.

    Rwanda nayo inapangana kutumia magari ya umeme kwa asilimia 100 mwaka 2050.

    Gari jipya hilo la e-Golf lina betri inayoweza kudumu kwa miaka 8 na inachukua saa moja tu kujaza umeme unaoweza kutumika kwa umbali wa kilomita 230.

    Maeneo 15 ya kuongeza umeme kwenye magari hayo yanatarajiwa kujengwa mjini Kigali.

    Kwa sasa magari ya majaribio ni manne na baadaye Volkswagen inatarajia kuyaongeza hadi 50.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako