• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwenyekiti wa Yanga kumfuta kazi kocha Zahera na benchi lake lote la ufundi hadi walinzi wa timu

  (GMT+08:00) 2019-11-06 09:01:18

  Habari iliyogonga vichwa vya habari kwenye soka Tanzania ni ile kuhusiana na kutimuliwa kazini kwa kocha wa klabu ya Yanga, hivyo jana mwenyekiti wa klabu hiyo Mshindo Msolla ilitangaza rasmi kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera pamoja na benchi lake lote la ufundi hadi walinzi wa timu hiyo. Zahera amefutwa kazi Yanga baada ya kuiongoza timu hiyo kwa jumla ya michezo 63 toka alipojiunga na Yanga April 2018, ameshinda michezo 32 na kupoteza michezo 21 sare mechi 10.

  Lakini saa chache baada ya kusambaa kwa taarifa hizo aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera amefunguka na kusema mwenyekiti Msolla amekiuka ahadi yake na hata barua ya kufukuzwa kazi hajapewa.

  Ndani ya msimu wa 2018/2019 Zahera ameiongoza Yanga kucheza jumla ya michezo 10 na kushinda mitatu, kufungwa minne na sare michezo mitatu, mkataba wa Zahera na Yanga ulikuwa unamalizika September 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako