• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Yemen na STC zasaini makubaliano ya kugawana madaraka

  (GMT+08:00) 2019-11-06 09:52:40

  Serikali ya Yemen na kamati ya mpito ya kusini STC zimesaini makubaliano ya kugawana madaraka huko Riyadh, Saudi Arabia.

  Habari kutoka televisheni ya Arabiya ya Saudi Arabia, zinasema, kutokana na msuluhishi wa Saudi Arabia, serikali ya Yeman na kamati ya mpito ya kusini wamesaini makubaliano ya Riyadh. Serikali ya Yemen itarudi mji mkuu wa muda Aden ndani ya siku saba, vikosi vyote vya Yemen vitasimamiwa na wizara za mambo ya ndani na ulinzi, na Yemen itaunda serikali ambayo itagawanya kwa usawa mikoa ya kusini na ya kaskazini.

  Mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman Al Saud, rais Abdu-Rabbu Mansour Hadi wa Yemen na mwenyekiti wa kamati ya kusini Aidarous Zubaidi wamehudhuria hafla ya kusaini makubaliano huko Riyadh.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako