• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ahutubia ufunguzi wa Maonyesho ya pili ya CIIE

  (GMT+08:00) 2019-11-06 09:54:54

  Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Uingizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE), na kutoa mapendekezo matatu kuhusu kuhimiza mafungamano ya kiuchumi duniani, kutangaza hatua tano muhimu za China katika kuendelea kusukuma mbele kiwango cha ufunguaji mlango kwa nje, na kuingiza msukumo wa China katika kujenga kwa pamoja uchumi wa dunia ulioko wazi duniani.

  Katika hotuba hiyo, rais Xi amezitaka nchi mbalimbali kujenga kwa pamoja uchumi wa dunia unaofungua mlango huku zikifanya ushirikiano, uvumbuzi na kunufaika kwa pamoja. Pia amesisitiza kuwa China itafungua mlango na kutoa fursa nyingi zaidi kwa nchi mbalimbali, kutoa mchango kwa ajili ya kuhimiza ujenzi wa uchumi wa dunia ulio wazi, na kujenga Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

  "Tunapaswa kushikana mikono wala si kuachana, kuongeza ushirikiano wala si kuweka vikwazo. Kupinga kithabiti kujilinda kibiashara na utaratibu wa upande mmoja. Nchi mbalimbali zinatakiwa kuimarisha uvumbuzi na ushirikiano, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ujuzi, kutafuta kunufaishana na kulinda kwa pamoja utaratibu wa kimataifa unaofuata msingi wa katiba na kanuni za Umoja wa Mataifa. Kuhimiza urahisishaji wa biashara na uwekezaji huria, na kuhimiza mchakato wa mafungamano ya kiuchumi duniani kupiga hatua kuelekea kufungua mlango zaidi, shirikishi, kunufaishana, na kupata mafanikio kwa pamoja, ili kuwanufaisha zaidi nchi na watu wao kutokana na mafanikio yaliyopatikana."

  Rais Xi amesisitiza tena kwamba, China itaendelea kushikilia sera ya kimsingi ya kufungua mlango, kuhimiza mageuzi, maendeleo na uvumbuzi kwa njia ya kufungua mlango, na kuendelea kuhimiza ufunguaji mlango kwa nje kwenye kiwango cha juu zaidi.

  "China ina soko kubwa, nawakaribisheni kuja kulishuhudia. China itaongeza umuhimu wa kimsingi wa matumizi ya ndani kwa maendeleo ya uchumi, kuweka mkazo mkubwa zaidi katika uagizaji bidhaa kutoka nje, kuhimiza maendeleo yenye uwiano kati ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa nje, biashara ya mizigo na utoaji wa huduma, biashara na uwekezaji kati ya pande mbili mbili, na kati ya biashara na viwanda."

  Hivi sasa China imesaini nyaraka 197 za ushirikiano katika kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na nchi 137 na mashirika 30 ya kimataifa. Rais Xi amesisitiza kuwa China itashikilia kanuni ya kujadiliana pamoja, kujenga pamoja na kunufaika kwa pamoja, na kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  "Tukitupilia macho siku za baadaye, China itashikilia wazo jipya la kujiendeleza, kuendelea kutekeleza mikakati ya kuhimiza maendeleo kwa njia ya uvumbuzi, kuandaa na kupanua msukumo mpya, kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya uchumi ili kuleta fursa nyingi mpya kwa ongezeko la uchumi duniani. Naamini kuwa mustakabali wa maendeleo ya uchumi wa China utakuwa mzuri zaidi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako