• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Harambee Starlets yaalika Zambia mechi ya kufuzu Olimpiki

    (GMT+08:00) 2019-11-06 17:56:27

    Mashabiki watakaofika uwanjani Kasarani kushabikia vipusa wa Harambee Starlets, katika mchuano wa kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki Tokyo, hawatatozwa kiingilio. Starlets watamenyana na vipusa wenzao kutoka Zambia siku ya Ijumaa, katika juhudi za kukata tiketi ya kushiriki michezo ya Olimpiki itakayofanyika nchini Japan mwaka ujao. Kwa mujibu wa vinara wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), kuondolewa kwa ada ya kiingilio ni uamuzi wa makusudi unalenga kuvutia mashabiki wengi zaidi kukishabikia kikosi cha Starlets. Mchuano huo utasimamiwa na refa Shamirah Nabaddah akisaidiwa na waamuzi wenzake wazawa wa Uganda – Jane Mutonyi, Nakitto Nkumbi na Florence Ayaro. Aline Bitagoye kutoka Burundi na Agar Mezing wa Cameroon watakuwa makamishna wa pambano hilo. Starlets watajibwaga ugani siku tatu tu baada ya kupepetwa 3-1 na chipukizi wa Kenya wasiozidi umri wa miaka 15, katika mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanjani Nyayo, Nairobi, hapo jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako