• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shughuli ya uteuzi wa timu ya Olimpiki kukamilika Juni 2020

  (GMT+08:00) 2019-11-06 17:57:40
  Kenya itawakilishwa na takriban wanamichezo 80 katika Michezo ya Olimpiki itakayoandaliwa jijini Tokyo, Japan kati ya Julai 24 na Agosti 9 mwaka ujao. Idadi hiyo ni nyongeza ya wanamichezo 13 zaidi, kutoka 67 waliopeperusha bendera ya taifa kwenye Olimpiki za 2016 zilizofanyika jijini Rio, Brazil. Msimamizi wa kikosi cha Kenya katika michezo hiyo, Bw Waithaka Kioni, alisema kuwa wanamichezo 45 wa Kenya tayari wamefuzu kwa mashindano hayo, ikiwa ni pamoja na waogeleaji wawili, wanariadha 28 na wanaraga wa timu ya taifa ya wanawake, Kenya Lionesses. Vikosi vingine vinavyotarajiwa kufuzu ni timu ya taifa ya soka ya wanawake (Harambee Starlets), timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande kwa wanaume (Shujaa), timu ya taifa ya voliboli ya wanawake (Malkia Strikers), timu ya taifa ya ndondi na baadhi ya wanariadha ambao uteuzi wao unatazamiwa kukamilika Juni 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako