• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanya biashara wenye ulemavu waomba msaada

  (GMT+08:00) 2019-11-06 18:04:54

  Wafanya biashara walemabu wataka watengenewe eneo kwa shughguli zao

  Kundi la wafanya biashara wenye Ulemavu (Uwalemba) katika mkoa wa Mbeya limeiomba serikali kuwasaidia na eneo kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zikiwamo sabuni na mafuta ya kupakaa.

  Katibu wa kundi hilo Ramadhani Shamte amesema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Reuben Mfune, alipotembelea na kuangalia shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazofanywa na kundi hilo.

  Shamte alisema wamejitahidi kuongeza uzalishaji wa bidhaa zao kwa kutumia teknolojia za kisasa lakini changamoto kubwa inayowakabili ni eneo kuwa finyu, hivyo kuomba kusaidiwa eneo kubwa ambalo litasaidia kupanua wigo wa uzalishaji.

  Alisema mbali na kuhitaji eneo kubwa la kufanyia shughuli zao, pia wana tatizo la masoko kwa kuwa licha ya kuzalisha kwa wingi bidhaa za mafuta ya kupakaa, sabuni za miche na maji hawana soko la uhakika kuuza bidhaa hizo.

  Shamte aliiomba serikali kuwatafutia soko la uhakika ili kuuza bidhaa zao ambazo alisema

  Alisema kiwanda chao ambacho kimepewa jina la Mbarali Soap hadi sasa kimetoa ajira kwa watu 12 ambao kati yao sita ni wenye ulemavu na sita hawana ulemavu.

  Aidha Mfune amewashauri wananchi na vikundi vingine kuchangamkia fursa za mikopo zinazotolewa na halmashauri huku akisisitiza asilimia 10 ya mapato ya ndani imetengwa kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya kinamama, vijana na wenye ulemavu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako