• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Kenya wakosa kupigia kura mswada wa riba ya benki kwa wateja

    (GMT+08:00) 2019-11-06 18:05:11

    Wakenya wamejipata katika hali ya zamani ambapo benki za kibiashara zilikuwa zikiwatoza riba ya hadi asilimia 30 kwa mikopo waliochukua.

    Hii ni baada ya wabunge wa Kenya kushindwa kutupilia mbali pendekezo la Rais Uhuru Kenyatta la kwamba sheria ya udhibiti wa riba iondolewe.

    Wakati suala hilo liliwasilishwa kupigiwa kura kulikuwa na wabunge 161 pekee bungeni ilhali kwa mujibu wa Katiba, kulihitajika thuluthi mbili za wabunge wote 349. Hii ina maana kuwa suala hilo lilihitajika kupigiwa kura na angalau wabunge 233.

    Kutokana na hilo, Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi hakuamuru wabunge wapigie kura suala hilo kwa sababu hakukuwa na idadi tosha ya wabunge ukumbini.

    Majuma mawili yaliyopita, Rais Kenyatta alikataa kuutia saini Mswada wa Fedha na kuurejesha bungeni na pendekezo kwamba kipengee kinachodhibiti riba inayotozwa na benki za kibiashara kiondolewe.

    Pendekezo hilo moja kwa moja lilibatilisha kipengee cha 33 (2) (a) cha sheria za Benki na ambayo inasema kuwa benki hazifai kutoza riba ya zaidi ya asilimia nne kuzidi kiwango kilichowekwa na Benki Kuu ya Kenya ambayo huwa ni asilimia tisa.

    Hii ina maana kuwa chini ya sheria hiyo, benki hazikufaa kutoza zaidi ya asilimia 13 kwa mikopo zinazotoa kwa wateja wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako