• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wavuvi haramu kufikishwa kotini

  (GMT+08:00) 2019-11-06 18:05:34

  Serikali ya Tanzania imesema kuanzia sasa haitawatoza tena faini wavuvi watakaokamatwa wakiendesha shughuli za uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu lililoko kati ya mikoa ya Kilimanjaro na Manyara, badala yake itawaburuza kortini.

  Uamuzi huo ulitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw Thomas Apson baada ya kunaswa kwa vyandarua vya kuzuia malaria vyenye thamani ya Sh. milioni 39.3 ambavyo vilikuwa vitumike kuvua mazalia ya samaki.

  Katika operesheni ya Jodari na Sangawe inayoendelea katika bwawa hilo, makokoro 12 na vyandarua vya malaria vimekamatwa na kuteketezwa.

  Apson alisema uvuvi haramu katika eneo linalozunguka Bwawa la Nyumba ya Mungu umekuwa ukishika kasi sana na hii ni kutokana na wavuvi hao haramu wanapokamatwa hutozwa faini na kisha kuachiwa huru.

  Mkuu huyo wa Wilaya alisema wananchi ambao wamekuwa wakifanya uvuvi haramu wamekuwa wakilitishia Jeshi la Polisi pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kuzuia biashara hiyo na mpaka sasa jumla ya watu kumi na nne wanashikiliwa kwa kutishia askari polisi.

  Alisema endapo wananchi watafanya uvuvi kwa kufuata sheria, serikali itawasaidia kupata soko la uhakika la uuzaji wa samaki ndani na nje ya nchi lengo likiwa ni kuinua maendeleo ya wananchi wanaozunguka bwawa hilo pamoja na Taifa kwa ujumla kwa kulipa kodi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako