• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wahimiza juhudi za makusudi kukabiliana na matukio makubwa ya afya ya umma barani Afrika

  (GMT+08:00) 2019-11-07 08:38:16

  Umoja wa Afrika umetoa mwito kwa nchi za Afrika na taasisi za Umoja wa Afrika kuwa na juhudi za makusudi kupambana na matishio ya afya kwa umma.

  Taarifa iliyotolewa na Umoja huo inasema hali ya afya ya umma kwa nchi za Afrika inaendelea kuboreka kwa kasi, lakini tishio la magonjwa bado ni kubwa. Taarifa imetaka kuongeza juhudi kwenye kukabiliana na hatari za afya zinazowakabili watu wa Afrika.

  Mwito huo umetolewa mjini Addis Ababa kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Afrika ulioandaliwa na kituo cha kupambana na magonjwa cha Afrika CDC, wakati washiriki wakijadili namna ya kuboresha mifumo ya afya ya umma ya taifa kwenye kukabiliana kwa haraka na magonjwa ya mlipuko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako