• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Malawi yafanya mazoezi ya kupambana na Ebola

  (GMT+08:00) 2019-11-07 08:38:39

  Serikali ya Malawi inafanya mazoezi ya kupambana na virusi vya Ebola kwenye eneo dogo la mpaka kati ya wilaya za Karonga na Chitipa kaskazini mwa nchi hiyo.

  Mazoezi hayo yanafanyika wiki tatu baada ya mgonjwa mmoja mwenye umri wa miaka 37 kufariki mjini Karonga mwezi uliopita akidhaniwa kufa kwa ugonjwa wa Ebola, na mamlaka za afya kukanusha vikali habari hiyo. Mtu huyo alionesha dalili kama za ugonjwa wa Ebola ikiwa ni pamoja na homa kali, kutokwa damu machoni, puani na mdomoni ambazo ni sawa na ugonjwa wa Ebola, na kifo chake kiliwatia hofu wamalawi wengi.

  Taarifa imesema mazoezi hayo yanafuatia maandalizi makubwa ya kupambana na ugonjwa wa Ebola na mpango wa mwitikio, ulioandaliwa na wizara ya afya ya Malawi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako