• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini na ubalozi wa China nchini humo wazindua kampeni dhidi ya Ukimwi

    (GMT+08:00) 2019-11-07 08:49:19

    Kampeni mpya dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi imezinduliwa nchini Sudan Kusini, ambayo inalenga kuongeza hatua za kinga na matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo.

    Kampeni hiyo ya mwaka mmoja inaongozwa na ofisi ya mke wa Rais wa Sudan Kusini Bibi Mary Ayen Mayardit kupitia shirika lake la hisani, Concern South Sudan, kwa kuungwa mkono na ubalozi wa China huko Juba.

    Kampeni hiyo ya kitaifa ya kukinga dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi inatetea kuhimiza tabia ya kujiepusha na ngono, uaminifu na matumizi ya mipira kama njia ya kujilinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako